Header Ads

Kenya yapeleka madaktari wa jeshi kuhudumu hospitali za umma



Madaktari wamekuwa kwenye mgomo nchini Kenya tangu JumatatuImage copyrightREUTERS
Image captionMadaktari wamekuwa kwenye mgomo nchini Kenya tangu Jumatatu
Kenya imepeleka madaktari wa kijeshi kwenye hospitali kubwa zaidi nchini humo ya Kenyatta, baada ya madaktari wa mwisho 300 waliokuwa wakifanya kazi kujiunga na mgomo unaoendelea ambao umeathiri huduma za afya kote nchini.
"Madaktari wetu tayari wako hospitalini kusaidia kesi za dhararu," alisema msemaji wa jeshi Paul Njuguna.
Tatizo hilo huenda likawa hata baya zaidi baada ya madaktari kutoka hospitali za kibinafsi na zile za kimeshenari, kusema kuwa watagoma kujiunga na mgomo huo wiki ijayo.
Mgomo huo wa kutaka nyongeza ya mishahara umesababisha maelefu ya madaktari na wahudumu wengine wa afya kususia kazi tangu siku ya Jumatu.
Wagonjwa ambao walihitaji huduma za dharura walikosa huduma na kubakia wakiwa wamelala hospitalini.

No comments