Header Ads

matoto wa miaka 6 kutumbikia kwenye karo la choo na kupoteza maisha

Image result for PICHA YA KISIMA CHA MAJI

simanzi imeibuka kwa wakazi wa mtaa wa bugwandege kata ya
ibinzamata  manispaa ya Shinyanga  baada Mtoto mariam jeremiah mwenye
umri wa miaka 6 mwananfunzi wa chekechea shule ya msingi ibinzamata
kutumbukia kwenye karo la choo na kupoteza maisha

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia radio faraja kuwa tukio hilo
limetokea jana  majira ya saa nane mchana ambapo mtoto Mariam na
wenzake  walikuwa wakicheza mchezo wa kukimbizana karibu na karo hilo
lililopo nyumba ya jirani ambapo  mtoto Mariam
alipitita juu ya mfuniko wa karo hilo  na kutumbukia


Pia mashuda hao akiwemo babu wa marehemu  wametupia lawama kwa
wajenzi wa choo hicho kujenga chini ya kiwango hali ambayo wanadai
imechangia kupoteza maisha kwa mtoto huyo.

                            

Kwa upande wake mwenyekit iwa serikali ya  mtaa huo AMAN ABDALAH
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wazazi kuwalinda
watoto wao na mazingira hatarishi ili kuepuka hajari zisizo za lazima 



No comments