Header Ads

msako wa madereva wa magari wanao kunywa pombe asubuhi


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga amejipanga kuanzisha utaratibu wa kuwapima madereva wa magari kwenye baa mbalimbali za jiji la Dar es salaam ili kuwakamata madereva ambao wanaanza kunywa pombe halafu wanaingia barababari kuendesha magari.
Akiongea Jumatatu hii katika kipindi cha Joto La Asubuhi cha EFM, Kamanda Mpinga amesema mpango huo utasaidia kupunguza ajali za barabarani ambazo zinasababishwa na unywaji wa pombe.
“Ni kweli watu wengi wanaendesha vyombo vya moto wakiwa wamekunywa pombe lakini hiyo changamoto inatokana na vifaa tulivyonavyo ni vichache lakini tunajihidi hivyo hivyo kuwapima,”alisema Mpinga.  “Kwa mfano kwa hapa Dar es salaam kwa kipindi hichi kunataka kuanzisha utararibu wa kuwapima watu kwenye mabaa. Yaani tunaweka gari nje ukitoka tu tunakupima,”
Katika hatua nyingine Kamanda Mpinga amewataka madereva kufuata sheria za usalama barabani ili kuepuka ajali ambazo zinaepukika.

No comments