Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi WILLIAM LUKUVI ameitaka idara ya ardhi katika mkoa wa Shiyanga kutoa hati
Waziri wa ardhi,nyumba
na maendeleo ya makazi WILLIAM LUKUVI ameitaka idara ya ardhi katika mkoa wa
Shiyanga kutoa hati ya umiliki wa viwanja
kwa wananchi ili kuiwezesha serikali kupata mapato.
Akizungumza na
watumishi wa idara hiyo katika kikao maalum kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga LUKUVI
amesema takwimu zinauonyesha mkoa wa Shinyanga kuwa una idadi kubwa ya watu
wenye viwanja vilivyopimwa lakini hawana hati za umiliki wa viwanja.
Amesema mpaka sasa mkoa
wa Shinyanga una idadi ya watu 1200 tu ambao wana hati miliki za viwanja vyao
jambo ambalo licha ya kuikosesha mapato serikali ambayo lingeyapata kupitia
kodi za majengo hali hiyo pia inawafanya wananchi wengi wakose mikopo kutoka
taasisi mbalimbali za kifedha.
WAZIRI
LUKUVI pia amewapiga marufuku maafisa wa ardhi kuchukua
viwanja au mashamba ya wananchi bila kuwalipa fidia inayoendana na thamani
halisi ya ya ardhi zao huku akiwataka
maafisa wanaohusika na mipango miji kuhakikisha wanaweka mikakati ya kupanga
mji kikamilifu ili kuepuka ujezi
holelela.
Walengwa wa TASAF awamu ya tatu Mpango wa kunusuru
kaya masikini mkoa wa Shinyanga wameombwa kutoa taarifa dhidi ya watendaji
watakaohusika kufanya hujuma hasa vitendo vya rushwa,katika utekelezaji wa
mpango huo
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Shinyanga bwana Dotto Maligisa amewaomba walengwa
kutoa taarifa Pale watakapobaini kuwepo udanganyifu wowote utakaofanywa na
watendaji zikiwemo kamati za usimamizi ngazi ya serikari ya mtaa,kitongoji na
kijiji,ikiwemo mianya ya rushwa.
Hatua hiyo ni kufuatia tetesi kutoka kwa baadhi ya
wananchi kwamba baadhi ya watendaji hutumia fursa hiyo kuwashawishi walengwa
kugawana nao Pesa wanazopokea kwenye mpango huo.
Mratibu huyo wa TASAF Mkoa wa Shinyanga amesema tayari
Mkoa wa Shinyanga umefanikiwa kuwafikia walengwa 34,883 kati ya 45,000
waliokuwa wametarajiwa.
Aidha amesema kati ya walengwa hao 641 wameondolewa
kwenye mpango kutokana na kukosa sifa.
Amesema
TASAF awamu ya tatu mpango wa kunusuru kaya masikini umeleta matokeo chanya
baada ya walengwa wengi kujikwamua kiuchumi katika maeneo ya kilimo,ufugaji na
ujenzi
Post a Comment