Header Ads

Darassa akifanya yake mbele ya wafanyabiashara wa Ilala.





Hit maker wa wimbo Muziki, Shariff Thabeet aka Darassa Jumatano hii alikutana na wafanyabiashara wa soko la Ilala Boma na kuonyesha baadhi ya vitu ambavyo ataenda kuvifanya Jumamosi hii kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Darassa akifanya yake mbele ya wafanyabiashara wa Ilala.
Darassa na Roma, kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano la Nichane Nikuchane.
Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa aliisimamisha Ilala pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni kionjo kabla ya shoo yenyewe kamili ya siku hiyo.
Akiongea na mashabiki wake, Darassa alisema amejipanga vizuri kuonyesha mambo mapya katika jukwaa hilo la burudani.
“Mashabiki zangu, siku hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar Live kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa nafanya miujiza kila ninapopanda jukwaani.” alisema Darassa.
Naye Meneja wa Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Abdallah Mrisho, alisema: “Shoo hii inayoenda kufanyika ni ya tofauti, kama tujuavyo Roma na Darassa kwa sasa ndiyo habari ya mjini hasa kwenye muziki wa Hip Hop, hii ni mara ya kwanza kwa Darassa kupanda kwenye Jukwaa la Dar Live, hivyo mashabiki ni fursa yenu kujumuika naye siku hiyo.”
Katika hatua nyingine, Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma Mbizo, alisema: “Kwa kiingilio cha Sh 5,000, mashabiki watapata fursa ya kuingia na kushuhudia mpambano huo mkali ambao rasmi utaanza saa 7 mchana mpaka majogoo.”
Mbali na wakali hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani ni pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature, Makhirikhiri, MC Darada, Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.

No comments