Serikali ya wilaya ya shinyanga imeahidi kutatua mgogoro wa ardhi
Serikali ya wilaya
ya shinyanga imeahidi kufuatilia na kuhakikisha inatatua mgogoro wa ardhi
uliopo katika mtaa wa Luhende kata ya Ndala
katika Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza na
wakazi wa mtaa wa Luhende katika kata ya Masekelo kwenye mkutano maalumu
uliokuwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi hao kuhusu mgogoro wa
ardhi,mwakilishi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,CHARLES MAUGILA amewaomba wananchi hao kuwa wavumilivu wenye subira
ili kutoa nafasi kwa watendaji kufuatilia ili kupata ufumbuzi.
Bwana MAUGILA
amesema kuwa viashiria vyovyote vya migogoro si ishara njema katika ustawi wa
maendeleo ya Jamii kwani inaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa Amani.Awali wakazi wa
mtaa wa Luhende kata ya Masekelo katika mkutano maalumu na maafisa kutoka ofisi
ya Mkuu wa wilaya na wale wa ardhi manispaa,wamelalamikia
kero ya mgogoro wa
ardhi ambao wamesema umesababishwa na maafisa wa ardhi kukosa uaminifu na
kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu
Wananchi hao
wameiomba ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na ofisi ya ardhi katika
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kushughulikia na kutatua kero zilizopo ili
kumaliza migogoro ya ardhi.
---
Kwa upande wake
afisa ardhi wa Manispaa ya Shinyanga bwana ALEX
RUTAHILWA amewaomba wananchi wote wenye migogoro ya ardhi kuhakikisha
wanazingatia taratibu zote zilizopo kisheria,ambapo pia ameshauri masuala
yote yaliyopo mahakamani yasijadiliwe kwa kuwa kila ngazi inafanya kazi
kwa mujibu wa miongozo.
Post a Comment