Header Ads

Jamii Mkoani Shinyanga imekumbushwa kuwa ina wajibu mkubwa

Image result for picha ya shinyanga

Jamii Mkoani Shinyanga imekumbushwa kuwa ina wajibu mkubwa  wa kuhakikisha inaweka mazingira salama kwa watu wenye albinism ili kuliwezesha kundi hilo kuwa huru lenye amani,katika nchi yao

Mwakilishi wa Jeshi la Polisi kamishina Msaidizi Mussa,ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuelimisha Jamii utakaotekelezwa na chama cha watu wenye ualbinism,ambapo amesema Jamii itambue umuhimu wa kuthamini Kundi hilo ili liweze kuwa huru,salama na lenye amani,kuliko hivi sasa ambapo wanauawa kutokana na imani Potofu.

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye albinism Mk
oa wa Shinyanga Mwalimu Martin Luben ameiomba Jamii kuthamini na kuheshimu utu wa albino kwani ni binaadamu wenye haki na mahitaji sawa na wengine,badala ya kuwa na hofu.

Mradi wa kuelimisha Jamii kuondokana na  imani Potofu za kishirikina zinazosababisha Mauaji ya watu wenye ualbino umezinduliwa leo kwenye Hotel ya Empire mjini Shinyanga na kuhusisha shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu SHIVYAWATA,Wadau,wanasheria Jeshi la Polisi,waganga wa Jadi na vyombo vya habari.

Mradi huo utatekelezwa na chama cha watu wenye ualbino Mkoa wa Shinyanga,chini ya ufadhiri wa Shirika la OPEN SOCIETY INITIATIVE FOR EAST AFRIKA,ambao utatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja katika mkoa wa Shinyanga.


No comments