Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga kuielimisha jamii
copy kwanye google
Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga wamesema wataendelea kuielimisha Jamii Juu ya Dhana ya
watu wenye ualbino ili Jamii iweze kufahamu na kuelewa kuwa kundi hilo lina
haki sawa na watu wengine.
Wameyasema hayo leo wakati wakijadiliana kwenye warsha ya
siku moja iliyofanyika kwenye hotel ya
Empire iliyopo mjini Shinyanga,kwamba ni wajibu wa vyombo vya habari
kuendelea kuifahamisha Jamii Juu ya
Madhara ya kuwaua albino, kwani kuwaua ni ukiukaji wa haki za binaadamu.
Afisa mahusiano wa
habari wa chama cha watu wenye ualbino
Tanzania JOSEPHAT TONA amesema Warsha hiyo ya siku moja imeandaliwa na chama
cha watu wenye ualbino ngazi ya Taifa kwa ufadhiri wa shirika la Open society foundations ikilenga kukutana na waandishi wa habari ili
kubadilishana mawazo,kujadili na kuona changamoto wanazokabiliana nazo watu
wenye ualbino na kisha kuona namna ya kuzitatua.
Post a Comment