JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime /Rorya linawashikilia watu wawili ambao ni ngariba
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime /Rorya linawashikilia watu wawili ambao ni ngariba kwa tuhuma za kuwakeketa wanafunzi wawili wanaosoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Nyankoni na kuwasababishia majeraha na maumivu makali.
Ngariba hao ni Angelina Kirimi (50) na Mwita Ryoba (54), wote wakazi wa kijiji cha Itiryo, tarafa ya Ingwe, wilayani Tarime.
Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, Andrew Satta alisema kuwa ngariba hao
walifanya vitendo hivyo vya kikatili vya kuwakeketa wanafunzi wawili wa
kike ambao majina yao yamehifadhiwa kati ya Desemba 5 na 7 mwaka huu.
Alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mashirika ya kupinga
ukatili na unyanyasaji kwa mtoto wa kike likiwemo la ATFGM la Kanisa
Katoliki Masanga, waliweza kuwabaini wanafunzi hao kukeketwa baada ya
wanafunzi hao kufanyiwa uchunguzi na Dawati la Jinsia na madaktari.
Kamanda alisema , “Watuhumiwa hao ambao ni ngariba tunawashikilia kwa
mahojiano zaidi na kisha tutawafikisha mahakamani kujibu tuhuma za
kudhuru mwili.
Jeshi letu linawaonya kwa wale wote wakaokamatwa
wakiwashawishi watoto wa kike kwenda kukeketwa wakiwemo wazazi,
wanaowapeleka kuwasindikisha watoto wa kike kwenda kukeketwa na
wakeketaji wenyewe ambao ni mangariba kama hawa tuliowakamata”.
Alisema ukeketaji unaofanywa kwa watoto wa kike umepigwa marufuku kwani ni moja ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Kamanda alisema wana taarifa za kitabibu kuwa wasichana waliokeketwa
hupata matatizo ya kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua na
kusababisha vifo na jamii inatakiwa kuacha mila zilizopitwa na wakati
ambazo zina madahara kwa jamii zikiwemo hizo za ukeketaji.
angalia video mpya ya vanesa mde na mmewe juma jux
angalia video mpya ya vanesa mde na mmewe juma jux
Post a Comment