Mamlaka nchini Ujerumani imewafungulia mashtaka vijana saba wakimbizi kwa jaribio la kutaka kumuua
Mamlaka nchini Ujerumani imewafungulia mashtaka vijana saba wakimbizi kwa jaribio la kutaka kumuua mtu asiye na makazi kwa kumchoma moto, wakati wa sikukuu ya Krisimas.
Washukiwa sita ambao wana kati ya miaka 15 na 18, walijisalimisha wenyewe baada ya polisi kuonesha picha zilizorekodiwa katika kamera ya uchunguzi, kuhusiana na shambulio hilo lililofanywa katika treni za chini ya ardhi mjini Berlin.
Hata hivyo mtu huyo hakudhurika.
Mshukiwa wa saba wa shambulio hilo, mwenye umri wa miaka 21, ambao polisi wanadai kuwa ndio mshukiwa mkuu, alikamatwa karibu na nyumbani kwake.
Watuhumiwa sita kati ya hao wanatokea Syria, huku mmoja akitokea Libya.
Wote hao walikwenda Berlin Ujerumani kama watu wanaotafuta makaazi mwaka 2014 na 2015.
Post a Comment