nyoka kujilaza kwenye maua ya Krismasi
Mwanamke mmoja amegundua nyoka yenye urefu wa mita moja iliokuwa imejipinda katika mti wa Krismasi nchini Australia.
Mwanamke huyo aliitisha usaidizi ili kuiondoa nyoka hiyo katika nyumba yake huko Melbourne,Victoria siku ya Jumapili.
Mtaalam wa kushika nyoka Barry Goldsmith alisema kuwa nyoka hiyo iliingia kupitia eneo la wazi katika mlango kabla ya kujipinda katika mapambo ya mti huo.
Nyoka za Tiger zinazopatikana katika pwani ya Australia zina sumu kali.
Bw Goldsmith alisema kuwa mwanamke huyo alichukua hatua madhubuti baada ya kuigundua nyoka hiyo.
Post a Comment