Klabu ya Yanga na Serikali wameingia mkataba kwa ajili ya klabu hiyo kuutumia Uwanja Mkuu wa Taifa
Klabu ya Yanga na Serikali wameingia
mkataba kwa ajili ya klabu hiyo kuutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na ule wa
Uhuru kwa ajili ya michezo yao ya Ligi Kuu Bara na ile ya Ligi ya
Mabingwa Afrika.
Mkataba huo kati ya serikali umesainiwa
leo na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Profesa Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Serikali na Kaimu Katibu Mkuu
wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit aliyeiwakilisha klabu hiyo kongwe
zaidi nchini.
Yanga imeruhusiwa kuvitumia viwanja hivyo kama viwanja vyake vya nyumbani lakini imetakiwa kuvitunza wakati wa matumizi.
Utunzaji huo, unahusisha mali pamoja na vifaa vyote ndani ya viwanja hivyo.
Iwapo kutatokea tatizo na hasa uharibifu, basi Yanga ndiyo wakaohusika na matengenezo kwa gharama yoyote.
Post a Comment