UCHUMI UMEKUWA MGUM MKOANI SHINYANGA
Kutokana na mvua kuchelewa kunyesha kwa wakati katika
Mkoani SHINYANGA imepelekea hali ya kiuchumi
kuwa ngumu katika msimu huu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka hali inayopelekea
wananchi kutopata mazao ya chakula kwa wakati
Wakizungumza na Redio Faraja FM kwa nyakati tofauti Baadhi ya
wananchi wametoa maoni yao juu ya hali ya kiuchumi katika msimu huu wa sikukuu
za mwishoni mwa mwaka na msimu wa
sikukuu za mwishoni mwa mwaka uliopita nakusema kuwa mazao ya chakula ndiyo wanayotegemea sana katika misimu yote ya
sikukuu za mwishoni mwa mwaka
Aidha wamesema sababu nyingine kubwa ambayo imesababisha
ugumu wa kiuchumi katika msimu huu wa sikukuu ni mfumko wa bei ambao pia
unasababishwa na ulipaji wa ushuru kwa wafanyabiashara wakati biashara
wanazofanya kuwa ngumu kutokana na wateja kukosa mazao ya chakula ambayo ndiyo
yanategemewa katika hali ya kiuchumi
pia wamesema kutokana na mfumko huo wa bei umesababisha
bidhaa nyingi kuadimika katika soko kuu la mjini
shinyanga na kupelekea watu wengi kubadilisha sehemu ya kufanyia mahemezi
na kuelekea katika soko la NGUZO NANE ambako wanaamini
kunaupungufu wa bei ya bidhaa hizo
hatahivyo wameiomba serikali kutoa punguzo la ushuru kwa
wafanyabiashara ilikuweza kushuka kwa bei ya bidhaa hizo na kuwafanya wananchi
kunufaika na huduma ya bidhaa zilizopo katika soko kuu mjini humo kwa kipindi hiki cha sikukuu za
mwishoni mwa mwaka
Post a Comment