Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania
Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa
blog .
Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia
blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo,
viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari .
Aidha,
Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo na
makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili
kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.
"Tuzo hizo
zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi hivyo
makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo
yatakayojielekeza kwenye nyanja tofauti" alisema Waziri Nape.Waziri Nape
pia alisema amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini
kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.
"Tutumie fursa
za kisiasa zilizopo, fursa za teknolojia ili kuhakikisha tiunajenga
Tanzania tunayoitaka, ishaurini Serikali kwa kutumia taaluma mliyonayo
ili kuweza kuipeleka nchi ya Tanzania tunayoitaka" alifafanua Waziri
Nape.
Post a Comment