Mtu mmoja mtembea kwa miguu amefariki papo hapo baada ya kugongwa na gari
ACP MULIRO JUMANNE MULIRO
Mtu mmoja mtembea kwa miguu amefariki papo hapo baada ya
kugongwa na gari na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea jana majira ya saa mbili na nusu
usiku katika eneo la buhangija kona kata ya ibinzmata katika manispaa ya shinyanga
Akitoa taarifa ya ajali hiyo kamanda wa jeshi la polisi mkoa
wa shinyanga MULIRO JUMANNE MULIRO
amemtaja aliyepoteza maisha kuwa ni KHADIJA PHILIPOmwenye umri wa miaka 25, mkazi wa ndembezi ambaye alikuwa
akitembea kwa miguu,na waliojeruhiwa ni
CHRISTINA SULEIMAN miaka 40, mkazi wa Nindo mtembea kwa
miguu,Pamoja na AGNESS NDAMA mwenye umri
wa miaka 25, mkazi wa Mwanza ambaye
alikuwa abiria katika gari hilo.
Kamanda murilo amesema katika uchunguzi wa awali
jeshi la polisi limebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa
gari hilo lenye namba za usajili T 247 ACX TOYOTA LAND-Cruza
Kwa upande wa mashuhuda a ajali hiyo wamesema kuwa mwendo
kasi wa dereva katika eneo la kona na ukosefu wa baadhi ya alama muhimu za barabarani
umechangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ajali hiyo
Aidha kamanda MULIRO amesema jitihada za kumpata dereva
ambaye ndio kiini cha ajali hiyo zinaendelea huku akitoa wito kwa madereva kuzingatia kanuni na
taratibu za barabari ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika
Post a Comment