Mbunge Chadema ataja dawa kukomesha mauaji ya albino
MBUNGE wa Viti Maalumu mkoani Simiyu, Gimbi Masaba (Chadema) amewataka viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini mkoani Shinyanga, kuongeza juhudi za kueneza injili ya neno la Mungu kwa wananchi ili kumaliza tatizo la mauaji ya wenye ualbino na vikongwe mkoani humo.
Masaba alizungumza hayo kutokana na chanzo kikuu cha mauaji ya watu hao wasio na hatia, kimekuwa kikitajwa kutokana na imani potofu za kishirikina, na hivyo kuwataka viongozi wa dini kueneza neno la Mungu ipasavyo, ambalo litasaidia kukomesha mauaji hayo.
Akizungumza kwenye harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya waimbaji wa kwaya ya Imani ya Kanisa la AIC Kata ya Kitangiri mjini Shinyanga, ambao wanatarajiwa kwenda Katavi kupeleka neno la Mungu, Masaba alisema viongozi wa kidini wana nafasi kubwa ya kumaliza mauaji ya watu hao.
“Ukiangalia chanzo kikuu cha mauaji ya watu hawa wasio na hatia ni imani potofu za kishirikina ambazo zinaweza kumalizwa na viongozi wetu wa kidini wa madhehebu mbalimbali kwa kutoa mahubili ya nguvu ambayo yatawafanya watu kumrudia Mungu wao,” alieleza mbunge huyo.
Pia aliwataka wananchi kujituma kufanya kazi kwa bidii ili kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na siyo kupenda njia za mkato ambazo zimekuwa zikisababisha mauaji ya watu wasio na hatia. Aliichangia kwaya hiyo Sh milioni moja na kuahidi kuwanunulia vyombo vipya vya muziki.
Pia aliwataka wananchi kujituma kufanya kazi kwa bidii ili kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na siyo kupenda njia za mkato ambazo zimekuwa zikisababisha mauaji ya watu wasio na hatia. Aliichangia kwaya hiyo Sh milioni moja na kuahidi kuwanunulia vyombo vipya vya muziki.
Mchungaji wa Kanisa hilo, David Kazimoto alilaani kitendo cha wananchi kuendeleza muaji ya wenye ualbino hasa vikongwe mkoani Shinyanga na kudai kuwa huko ni kukeuka amri 10 za Mmungu ambazo zinamzuia mtu kutomtoa uhai mwenzake. Aliahidi kupanga mikakati ya kutoa neno la Mungu juu ya kupinga mauaji hayo.
video la kwata la kimya kimya angalia hapojini
Post a Comment