Serikali ya mtaa wa Dome kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga imekabidhi kwa Jeshi la Polisi Vitu mbalimbali
Serikali ya mtaa wa Dome kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga imekabidhi kwa Jeshi la Polisi Vitu
mbalimbali zikiwemo nguo zinazoshabihiana na sare za askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ,ambavyo
vilitelekezwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wahalifu.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa afisa Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Inspekta
ZAINABU MANGALA,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jumamosi Disemba 17, Mwenye kiti wa mtaa wa Dome SOLOMONI NALINGA, amesema kuwa vitu
hivyo zikiwemo nguo zinazoshabihiana na sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania J.W.T.Z, mita ya maji moja ,mashuka mawili, nondo moja ,baskeri tano vilitelekezwa na watu wasiofahamika wanaosadikiwa kuwa ni wahalifu.
-
Mwenyekiti huyo amewaomba wananchi kutoa Taarifa pale
wanapobaini kuna viashiria vya watu wahalifu katika eneo hilo pia awetaka wananchi kuenderea kufanya dolia kila siku ilikuzuia hualifu.
Kwa upande wake Afisa
huyo wa Jeshi la Polisi insipekta ZAINABU
MANGALA amepongeza Jitihada zilizopo baina ya viongozi na wakazi wa mtaa wa Dome katika suala la kuimarisha ulinzi na usalama
wa mali na raia.
Afisa huyo wa Jeshi la Polisi amewaomba wananchi kutoa
taarifa Pale wanapobaini kuwepo
viashiria vya uhalifu.
Post a Comment