Header Ads

Simba SC kikitarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumatano kuiva timu ya Al-Masry inayotoka nchini Misri,

Katika kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo kikosi cha Simba SC kikitarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumatano kuiva timu ya Al-Masry inayotoka nchini Misri, Ofisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara amezungumzia hali ya wachezaji wake muhimu na wakutumainiwa, Emmanuel Okwi, John Bocco na Haruna Niyonzima.
 

Benchi la ufundi letu likaona kwa hali ya Okwi na Bocco wangeweza kucheza jana lakini wakachukua tahadhari kwakuwa tunamechi kubwa zaidi siyo kwamba tulikuwa tumeizarau mchezo ule hapana lakini kucheza kwao ilikuwa hatari zaidi walitakiwa wapumzike vizuri.
Kutokucheza kwao ni kwasababu ya kucheza siku ya Jumatano kwa hiyo kuwepo kwao kutakuwa kwa asilimia 100 Insha Allah kwahiyo watakuwepo.
Haruna Niyonzima amesharejea taarifa nilizo nazo hakufanyia tena operesheni lakini matibabu yake yalikuwa ni tiba ya hali ya juu.
Kikosi cha Simba kimeingia kambini hii leo mara baada ya kutoka sare ya mabao 3 – 3 dhidi ya Stand United katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo timu hiyo ikiongoza katika msimamo kwa kuwa na jumla ya pointi 46 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Yanga SC wenye alama 40 na mchezo mmoja mkononi.

No comments