Header Ads

Mgombea urais mwenza wa chama cha Republican nchini Marekani Mike Pence na mwenzake wa Democratic Tim Kaine wamelumbana kuhusu taarifa za kodi za Donald

Mgombea urais mwenza wa chama cha Republican nchini Marekani Mike Pence na mwenzake wa Democratic Tim Kaine wamelumbana kuhusu taarifa za kodi za Donald Trump kwenye mdahalo wa runinga..

Pence na KaineImage copyrightREUTERS
Image captionBw Pence amesema Trump alitumia "werevu" kukwepa kulipa kodi
Mgombea urais mwenza wa chama cha Republican nchini Marekani Mike Pence na mwenzake wa Democratic Tim Kaine wamelumbana kuhusu taarifa za kodi za Donald Trump kwenye mdahalo wa runinga..
Bw Pence, ambaye ni gavana wa Indiana, amesema mgombea urais wa chama cha Republican Bw Trump alitumia "werevu" katika kutumia sheria za kodi kukwepa kulipa kodi.
Lakini Bw Kaine, seneta wa Virginia, alipinga wazo hilo la "werevu" akishangaa iwapo ilikuwa busara kukwepa kulipa pesa za kutumiwa kulipa wanajeshi au kufadhili elimu shuleni.
Bw Trump ameshutumiwa sana kutokana na rekodi yake ya ulipaji kodi.
Amekataa kufichua taarifa zake za ulipaji kodi lakini gazeti la New York Times majuzi lilifichua kwamba huenda amekwepa kulipa kodi kwa miaka 18 iliyopita.
Hili liliwezekana kwa sababu bw Trump, aliyewekeza katika biashara ya ujenzi na uuzaji wa hoteli, alipata hasara kubwa ya zaidi ya $900 milioni mwaka 1995.
Hajakanusha habari hizo.
Akimshambulia Bw Trump, Bw Kaine alisema: "Nafikiri sote tunaofanya hivyo 

No comments