Mito imeanza kukakuka, ekari zaidi ya 13,00 za misitu kuharibiwa na hofu ya barafu kutoweka katika miongo michache ijayo barani Afrika ikiwa ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira UNEP.

Ili kulinda mazingira na kuepuka athari za mabadiliko hayo, ripoti ya UNEP iliyozinduliwa nchini Uganda kwenye kongamano kuhusu milima duniani, inasema ni lazima hatua za msingi za upandaji miti zichukuliwe kuokoa kizazi cha sasa na kijacho.Ripoti hiyo "Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, uhifadhi wa mazingira na mali asili" inasema mlima Kilimanjaro ulioko nchini Tanzania ni chanzo muhimu cha maji kwa wakazi wa Kilimanjaro lakini pia kujaza mto Pangani ambao husaidia kwa chakula, mafuta na zana za ujenzi kwa sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki.
Tangu mwaka 1976 miti inaendelea kupungua kwenye mlima Kilimanjaro, na athari zake sasa zinadhihirishwa na uhaba mkubwa wa maji ambao unawakumba wakazi wa mkoa huo na hususani mji wa Moshi.
Post a Comment