Header Ads

Saida Karoli anaogopa kugusa hata jani, akidhani ni nyoka anayetaka kumng’ata.

Saida Karoli anaogopa kugusa hata jani, akidhani ni nyoka anayetaka kumng’ata.
saida-karoli
Ni kwasababu licha ya kufanya vizuri kimuziki miaka kadhaa iliyopita, hakupata chochote na bado anaishi katika mazingira magumu.
“Niliumizwa kuanzia mwanzo, ni vitu vichache nilivyovipata, kama mkibahatika waandishi wa habari wenye makamera na wakija kwangu watashuti kulingana na nilivyo, wataona mazingira ninayoishi ndipo watanzania watazidi kufunguka zaidi,” Saida alimwambia mtangazaji wa Jembe FM, Natty E.
Kwa sasa Saida Karoli anaishi jijini Mwanza. Hivi karibuni amerejea tena kwenye midomo ya watu baada ya Diamond kurudia wimbo wake Salome.

No comments