Aliyekuwa mchezaji wa Chelsea Didier Drogba alikataa kuichezea Montreal Impact baada ya kuambiwa hataanzishwa dhidi ya Toronto ,kulingana na kocha Mauro Biello.
Aliyekuwa mchezaji wa Chelsea Didier
Drogba alikataa kuichezea Montreal Impact baada ya kuambiwa
hataanzishwa dhidi ya Toronto ,kulingana na kocha Mauro Biello.
Montreal hapo awali ilikuwa imesema kuwa Drogba alikuwa anauguza jeraha la mgongo na hivyobasi asingeweza kucheza.
Lakini Biello alisema: Hakukubali kwamba angechezeshwa kama mchezaji wa ziada na mwishowe hakutaka kushirikishwa katika kikosi cha watu 18.
Kocha huyo aliongezea: Alikuwa na tatizo katika mgongo wake lakini alikuwa anaweza kucheza.
Drogba ambaye aliondoka Chelsea mwezi Julai 2015 amekuwa akitumiwa kama mchezaji wa ziada katika mechi mbili kati ya nne.
Amefunga mabao 10 katika mechi 21 msimu huu.
Post a Comment