Header Ads

Moja kati ya marapa wakali nchini Tanzania Stereo ametoa pongezi kwa rapa mwenzake Nikki wa Pili kwa kuendelea na PHD huku na yeye akifuata nyayo zake kwa kusema anataka kwenda kuchukua elimu ya PHD pia.

Kwa kupitia eNewz, Stereo amesema kuwa kwa sasa ana elimu ya degree lakini hatasita kuitafuta elimu ya PHD huku akimpongeza Nikki wa Pili kwa kuweza kuwa chachu kwa wasanii wengine akiwemo yeye kutamani kusonga mbele kielimu.
“Nampongeza sana Nikki wa Pili kwa uamuzi wake wa kujiendeleza na PHD amenihamasisha sana hivi karibuni na mimi nitajiendeleza kielimu kwa kuwa kwa sasa nina degree na Mungu akijalia nifikia hatua ya PHD'.
Hata hivyo Stereo amemalizia kwa kuwashauri wasanii wenzake kujipanga vyema hasa katika maswala muhimu ya elimu kwa kuwa elimu inasaidia sana hata katika maswala ya muziki wao kwa kuwa muziki ni biashara ambayo inakuwa kwa kasi sana.
Nikki wa Pili

No comments