angalia video la gari lilivyo angukia nyumba old shinyanga
gari lilivyo angukia nyumba hiyo angalia video hiyo
\
kijiko likijaribu kulitoa gari hilo kwenye nyumba
Mtu mmoja aitwaye JULIUS MWANDU mkazi wa OLD SHINYANGA katika manispaa ya Shinyanga amenusurika kifo baada ya Lori la kusomba mchanga kuparamia nyumba yake wakati akiwa amelala.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa mbili asubuhi baada ya tela la gari hilo lililokuwa likimwaga mchanga jiarani na nyumba yake kufyatuka na kuaparamia sehemu ya nyumba hiyo.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo wamesema tela la gari hilo lilifyatuka na kuingia katika chumba alichikuwa amelala Bw.JULIUS lakini alifanikiwa kutoka kabla ya ukuta wa nyumba kuanguka.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo ingawa baadhi ya vitu ikiwemo baiskeli na kitanda vimeharika vibaya baada ya kupondwa na na ukuta wa nyumba.
Dereva wa gari hilo lenye namba za usajili T.821 AYM alifanikiwa kukimbia mara baada ya tukio hilo kutokea.
Mwenyekiti wa kijiji cha OLD SHINYANGA DOTTO BWIRE amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
nyumba ya juliasi mwandu
gari lilolo anguka
Post a Comment