Header Ads

Chanjo mpya dhidi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi itaanza kufanyiwa majaribio nchini Afrika Kusini Jumatano wiki hii.


Matokeo ya majaribio hayo yanatarajiwa kutolewa mwaka 2020

Chanjo mpya dhidi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi itaanza kufanyiwa majaribio nchini Afrika Kusini Jumatano wiki hii.
Wanasayansi wanasema huenda ikawezesha binadamu kukabiliana na virusi hivyo iwapo itafanikiwa, shirika la habari la AP linasema.
Wakati wa majaribio hayo, ambayo yamepewa jina HVTN 702, wanasayansi wanatarajiwa kuwatumia wanaume na wanawake 5,400 ambao wanashiriki ngono kutoka maeneo 15 nchini Afrika Kusini.

Washiriki hao watakuwa wa umri wa kati ya miaka 18 na 35.
Majaribio hayo yatakuwa makubwa zaidi na ya kina zaidi ya chanjo ya Ukimwi kuwahi kufanyika nchini Afrika Kusini ambapo zaidi ya watu
"Ikitumiwa pamoja na silaha tulizo nazo sasa za kuzuia maambukizi, chanjo hiyo inaweza kuwa msumari wa mwisho katika jeneza la Ukimwi,"
Anthony Fauci, mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Maradhi ya Kuambukizana na Mzio ya Marekani (NIAID) amesema kupitia taarifa.
"Hata kama mafanikio yake yatakuwa ya kadiri, hilo linaweza kupunguza pakubwa mzigo unaotokana na maradhi hayo katika nchi zenye viwango vya juu vya maambukizi, mfano Afrika Kusini."
Chanjo ambayo itafanyiwa majaribio chini ya HVTN 702 ina uhusiano na majaribio ya chanjo yaliyofanywa mwaka 2009 nchini Thailand.

Chanjo iliyofanyiwa majaribio mwaka huo iligunduliwa kuwa na mafanikio asilimia 31.2 katika kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika kipindi cha ufuatilizi cha miaka 3.5 baada ya mtu kupewa chanjo.
Virusi vya HIV huua kinga yote ya mwili na kuacha mwili kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi mengine.

No comments