Header Ads

silaha zote zilizosajiliwa nchini










Image result for picha ya bunduki

JESHI la Polisi nchini limesema asilimia 40.82 ya silaha zote zilizosajiliwa nchini na hivyo kutoa mwezi mmoja kwa wasiohakiki silaha hizo kuzihakiki vinginevyo watafutiwa leseni ya umiliki, kutangazwa kwenye vyombo vya habari na kufikishwa mahakamani.

Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Boaz alisema hayo jana jijini Dar es Salaam kuwa wamiliki ambao hawajahakiki silaha hizo kwa sababu mbalimbali wanatakiwa kufika katika vituo vya polisi kuhakiki kuanzia Novemba 21 mwaka huu hadi Desemba 20, mwaka huu.

Alisema baada ya zoezi la uhakiki silaha kukamilika, tathmini inaonesha ni asilimia 59.18 pekee ndizo zimehakikiwa. Serikali ilifanya uhakiki wa silaha zote za kiraia Tanzania bara kuanzia Machi 22 mwaka huu hadi Juni 30 mwaka huu.

Aidha alitoa mwito kwa wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha silaha hizo katika vituo vya polisi au ofisi za Serikali za mitaa kwani atakayesalimisha silaha hatachukuliwa hatua za kisheria. mwisho



 chanzo habari leo

No comments