Idadi ya vifo vilivyosababishwa na ugaidi imeongezeka mara sita zaidi katika nchi zilizoendelea kwa mwaka 2015
Idadi ya vifo vilivyosababishwa na ugaidi imeongezeka mara sita zaidi katika nchi zilizoendelea kwa mwaka 2015, wakati mashambulizi yanayochochewa na kundi lenye itikadi kali linalojiita Dola la Kiislamu IS yakizidi kusambaa duniani, kwa mujibu wa takwimu za ugaidi dunia.
Wakati uingiliaji wa kijeshi dhidi ya IS na Boko Haram ulipunguza vifo vinavyotokana na ugaidi kwa asilimia 32 katika nchi za Iraq na Nigeria, takwimu zinaonyesha kwamba vifo vya aina hiyo katika nchi za jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo OECD viliongezeka kutoka 77 mwaka 2014 hadi 577 mwaka 2015.
Vifo vingi vilitokea nchini Uturuki na Ufaransa ambako kulishuhudiwa mashambulizi makubwa ya kigaidi. IS imepanua wigo wake duniani ikiyalenga mataifa 28 mwaka 2015 kutoka nchi 13 mwaka 2014 na pia ilifanya jumla ya mashambulizi 252 katika miji tofauti yaliyowaua watu 6141 mwaka jana.
MTU WANGU WA NGUVU KAMA ULIPITWA NA HII KUHUSU AJARI ILIYO TOKEA MKOANI SHINYANGA ANGALIA VIDEO HII LIKE UKURASA WETU WA KALI ZOTE BLOG
Post a Comment