Serikali,wadau na viongozi wa dini wameshauriwa kutoa elimu zaidi kwa jamii ili iondokane na imani potofu
Serikali,wadau na viongozi wa dini wameshauriwa kutoa elimu zaidi kwa jamii ili iondokane na imani potofu
Serikali,wadau na
viongozi wa dini wameshauriwa kutoa
elimu zaidi kwa jamii ili iondokane na imani potofu zinazochangia mauaji ya
watu wenye ualbino.
Wito huo umetolewa leo
na washiriki wa mdahalo wenye lengo la kupinga mauaji kwa watu wenye ualbino
uliokuwa umeandaliwa na Radio Faraja kwa kushirikiana na shirika la THE
FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY la jijini DAR-ES-SALAAM.
Washiriki wa mdahalo
huo kwa pamoja wamesisitiza kutolewa kwa elimu zaidi katika jamii ili iwe na
ufahamu kuhusu sababu za mtu kuzaliwa katika hali ya ualbino ili kuondoa
mitazamo hasi kwa kundi hilo ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya watu kuamini
kuwa viungo vyao vinaweza kuwasaidia kupata mafanikio.
Pia wamependekeza jamii
kushirikishwa kikamilifu katika suala la ulinzi na usalama hali ambayo
itasaidia kuwabaini wanaojihusisha na mauaji hayo ikiwemo waganga wa kienyeji
wanaopiga ramli chonganishi.
Naye mwakilishi wa
kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SP.SHABU B.SHABU amesema jeshi hilo haliwezi kufanikiwa kukomesha
mauaji hayo peke yake, endapo jamii
itaendelea kutotoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu wanaopanga mipango
ya kufanya mauaji hayo na kutokuwa tayari kutoa ushahidi pale watuhumiwa
wanapokamatwa.
-
Post a Comment