watu zaidi ya 99 wafariki kwenye ajali ya treni India
watu zaidi ya 99 wafariki kwenye ajali ya treni India
Idadi ya watu waliyofariki kutokana na ajali ya treni iliyotokea mapema leo kaskazini mwa India, imeongezeka hadi tisini na tisa na kuwajeruhi mamia ya wengine.
Treni hiyo ilikuwa ikitoka Indore kuelekea Patna kabla ya kupoteza muelekeo na kutoka katika barabara ya reli na kuanguka ilipokaribia mji wa Mashariki wa Kanpur katika jimbo la Utter Pradesh.
Maafisa wa kutoa huduma za dharura wanajaribu kuwaokoa manusura waliokwama katika mabehewa yaliyoanguka.
Waziri wa uchukuzi wa India ameamuru kufanywa kwa uchunguzi kubaini kilichosababisha ajali hiyo.
chanzo bbc
Post a Comment