WAKAZI WA SHINYANGA WA PINGA JESHI LA POLISI
KAMANDA MKOA WA TABORA
Baadhi ya wakazi katika Manispaa ya shinyanga wamekuwa na
maoni tofauti kuhusu hatua iliyochukuliwa na Jeshi la Polisi nchini kuwaondoa
kwenye vitengo askari wa usalama barabarani
kutokana na uzembe uliosababisha vifo na majeruhi.
Wakizungumza na KALI ZOTE BLOG kwa nyakati tofauti leo wamesema
ajali iliyotokea katika barabara ya Tabora -shinyanga eneo la kijiji cha
nsalala kata ya tinde wilaya ya shinyanga imechangiwa na uzembe wa dereva,kondakta na abiria
kushindwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani
Wamesema licha ya Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kinidhamu
kwa maaskari wa kitengo cha usalama barabarani waliokuwa zamu siku hiyo,lakini
chanzo kikubwa ni uzembe wa dereva na kondakta wake kubeba abiria wengi kuliko
mahitaji ya gari.
Mmoja wa wananchi waliozungumza na redio faraja leo mjini
Shinyanga Wesenslaus Modest amekuwa
na maoni tofauti ambapo amesema kuwa Jeshi la Polisi kuchukua hatua za
kinidhamu dhidi ya askari wake wa kitengo cha usalama barabarani waliokuwa zamu siku hiyo ni sahihi kwa
kuwa hawakuwajibika katika majukumu
yao,hali iliyopelekea kutokea ajali
Novemba 07,mwaka huu katika barabara
ya Tabora Shinyanga,eneo la kijiji cha nsalala kata ya Tinde wilaya ya
shinyanga Watu 18 walifariki dunia na
wengine watatu kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana
Huku Chanzo cha ajali hiyo kikielezwa
kuwa ni uzembe wa dereva wa NOA ambaye alitaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele
yake katika eneo la hatari.
KAMANDA MKOA WA SHINYANGA
Post a Comment