Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameonya madiwani
Mkuu wa wilaya
ya Shinyanga Josephine Matiro ameonya madiwani wa halmashauri ya manispaa ya
Shinyanga kujitengeneza vikao kiholela ambavyo havina tija kwa madhumuni ya kujipatia
Posho.
Matiro
amezungumza haya leo kwenye baraza la dharula la madiwani hao lililokuwa na
ajenda moja kuu ya kujadili taarifa za ubovu wa Grade lillilokuwa likituhumiwa
na baadhi ya madiwani hao kuwa haliwezi
kufanya kazi ambalo limegharimu milioni 520.
Matiro amesema
baada ya kusikiliza majadiliano ya Greda hilo amebaini tatizo hilo kila diwani
analifahamu, ambalo lilipaswa kuisha kwenye kikao kilichopita cha Oktoba 28 na
29, lakini anasiitika kwa madiwani hao kuchezea fedha ambazo zilipaswa
kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.
Aidha kufuatia
kikao kikao mkuu wa wilaya amemonya mkurugenzi wa manispaa hiyo Lewis Kalinjuna
kuwa endapo akirudia kuruhusu vikao vya namna hiyo vya kujitengenezea mazingara
ya posho serikali haita sita kumwajibisha.
Kwa upande wake
naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akitoa taarifa ya juu ya
Greda hilo mara baada ya madiwani kujigeuza kuwa kamati, wamekubariana Greda
hilo ni zima isipokuwa walichokosea ni kumpatia mtu wa kulitumia ambaye
hajalisomea.
Pia amesema
kutokana na tatizo hilo hivyo wameridhia kupeleka watu wawili kwenda kulisomea
Greda hilo ambalo litafanya kazi mbalimbali za halmashauri ya manispaa ikiwamo
uchongaji wa barabara.
Mtambo huo wa
Greda ulinunuliwa mwaka jana Marchi 20, lakini kutokana na kukaa muda mrefu
kwenye ofisi za halmashauri hiyo kwa kukosa Opareta wa kulitumia na lilionekana
kuwa bovu na hivyo Madiwani kuingiwa na
hofu kuwa pesa za mtambo huo zimeliwa.
Post a Comment