David Nkulila amejiuzuru nafasi ya ujumbe kwenye kamati ya Fedha na utawala kwa kile alichokieleza ameshindwa kukubaliana na baadhi ya mambo yanavyoamuliwa
Diwani wa kata ya
Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga David
Nkulila amejiuzuru nafasi ya ujumbe kwenye kamati ya Fedha na utawala kwa
kile alichokieleza ameshindwa kukubaliana na baadhi ya mambo yanavyoamuliwa
katika kamati na baraza.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari kwenye kikao maalumu
kilichofanyika kwenye klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga mjini
hapa.
Mheshimiwa Nkulila
amesema hatua ya kujiuzuru kwake katika nafasi hiyo ni ishara ya kutokubaliana
na na baadhi ya mambo ambayo yanakiuka sheria,kanuni na taratibu.
Ameyataja baadhi ya
mambo yaliyosababisha yeye kujiuzuru katika kamati hiyo ya Fedha na utawala
kuwa ni Pamoja na udanganyifu uliofanyika ambapo baraza la madiwani la manispaa
ya Shinyanga liliandaa bajeti na kuiwasilisha wizarani,kutotekelezeka kwa
sheria ya ujenzi wa nyumba za ghorofa kutokana na mianya ya rushwa,lakini
mgogoro wa greda,hoja za barabara za lami ambapo ambapo zimekuwa zikitajwa
kilometa nyingi tofauti na uhalisia.
Diwani nkulila
amesema amefikia uamuzi wa kujiuzuru katika nafasi hiyo ya ujumbe wa kamati ya
fedha na utawala, baada ya kutafakari kwa kina Juu ya utata kuhusu mambo kadhaa
yanayojitokeza katika Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ambayo ni kinyume na
matarajio lakini pia yana athari kwa
wananchi ambao walimwamini na kumpa
dhamana ya uongozi.
Mheshimiwa Nkulila akizungumza na waandishi wa habari
Post a Comment