Waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif leo Jumatano atakagua mazoezi ya kijeshi
Waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif leo Jumatano atakagua mazoezi ya kijeshi yaliyoanza mpakani mwa nchi hiyo na India, wakati mvutano baina ya mataifa hayo mawili yenye silaha za nyuklia kuhusu eneo linalozozaniwa la Kashmir ukizidi kuongezeka.
Ndege za kivita, vifaru na mizinga mikubwa inatarajiwa kutumika katika mazoezi hayo katika eneo la Kahipur Tamewali kilometa 50 kutoka mpakani. Mazoezi hayo yanafanywa ikiwa ni siku mbili baada ya askari saba wa Pakistan kuuawa katika mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na vikosi vya India.
Mwezi Septeba askari 19 wa India waliuawa katika eneo la Kashmir na kuuzidisha mvutano baina ya nchi hizo mbili, ambapo India iliwatupia lawama wanajihadi wanaoendesha shughuli zao nchini Pakistan, madai ambayo yalikanushwa na Pakistan.
Post a Comment