Header Ads

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza


Image result for picha ya Mwigulu Nchemba



WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke na kumhakikishia ushirikiano zaidi kati ya wizara yake na Ubalozi huo nchini.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo, mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu jijini Dar es Salaam ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na Ofisi ya Balozi huyo nchini.
Mwigulu alimhakikishia balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.
“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Mwigulu.

Hata hivyo, Balozi Sarah alimshukuru Waziri Mwigulu kwa mazungumzo waliyoyafanya na kumhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Uingereza na Tanzania.

No comments