Header Ads

yanga kushusha pumzi sasa

yanga kushusha pumzi sasa
Image result for picha ya yanga



KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi ameshusha pumzi akisema wanashukuru kwa kumaliza mzunguko wa kwanza kwa ushindi wenye matumaini ya kurudi katika nafasi yao.

Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara juzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ushindi huo unaipa nafasi Yanga kuweka matumaini yake ya kutetea taji la ubingwa kwa kufikisha pointi 33, akitofautiana kwa pointi mbili na kinara wa ligi wekundu wa Msimbazi, Simba wenye pointi 35.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Mwambusi alisema mchezo wa mwisho ulikuwa ni migumu, lakini muhimu kwao ilikuwa ni kupata pointi na hilo lilifanikiwa.
“Tunamshukuru Mungu kwa kumaliza mchezo wetu wa mzunguko wa kwanza kwa ushindi. Mchezo ulikuwa mzuri na mgumu, tuliwaambia wachezaji kuwa makini na kushinda kwa sababu tuliongozwa, kama tungewapa nafasi wapinzani basi ingekuwa ngumu kushinda,”alisema.

Mwambusi alisema sasa wanaangalia namna ya kujipanga kwa mzunguko wa pili kwa kuhakikisha wanarudi na kasi waliyomaliza nayo na kulitetea taji lao.
Kwa upande wake, Kocha wa Ruvu Shooting S
eleman Mpungwe alisema walijipanga kushinda kwa mbinu zote, lakini ilishindikana baada ya Yanga kuonesha ugumu kwa kuwashambulia na kutumia makosa yao kuwafunga.

“Mchezo ulikuwa mzuri na wenye ushindani, lakini mwisho wa siku tumefungwa, tulikuja na mbinu zetu za kuwamaliza, tulishindwa kudumu nazo tukafungwa,”alisema.

Alisema kupoteza katika mchezo huo haimaanishi kuwa timu yake ina mapungufu, isipokuwa kilichotokea ni sehemu ya mchezo na kuahidi kuyafanyia kazi kasoro zao ili kufanya vizuri michezo ijayo ya mzunguko wa pili.

No comments