madaktari bingwa 17 kutoka nchini Saudi Arabia, wapo watua tanzania
madaktari bingwa 17 kutoka nchini Saudi Arabia, wapo watua tanzania
JOPO la madaktari bingwa 17 kutoka nchini Saudi Arabia, wapo Visiwani Zanzibar tangu jana wakitoa matibabu bure katika hospitali za Chake Chake na Wete, Kisiwani Pemba.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemed Mgaza alisema madaktari hao wamekuja kwa ufadhili wa Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana wa Kiislamu ya Saudi Arabia (World Assembly of Muslim Youth (WAMY).
“Madaktari hao wameanza kutoa huduma leo (jana) na ratiba yao itahitimishwa Novemba 22 na ni jambo la kujivunia kwa wataalam hao kuamua kwenda nyumbani Tanzania kutumia taaluma zao,” alisema Balozi Mgaza.
Alisema pia madaktari hao watatoa huduma bila malipo na wamekuja na dawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali ambavyo mwisho wa kambi hiyo watavitoa msaada kwenye hospitali hizo.
Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, ni mara ya kwanza kwa madaktari hao kuja Tanzania na wanatarajiwa kutoa huduma hizo sehemu nyingine za Tanzania siku zijazo baada ya kukamilisha awamu ya kwanza. Madaktari hao wameshatoa huduma kama hizo katika nchi za Comoro na Cameroon.
Post a Comment