TASAF awamu ya tatu kutumia fedha kwa malengo yaliyokusudiwa
MKUU WA MKOA SHINYANGA Zainabu Telack
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Zainabu Telack amewaomba
walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF awamu ya tatu kutumia fedha
kwa malengo yaliyokusudiwa badala ya kutumia kwenye mambo ya anasa
Ameyasema hayo Jana wilayani kishapu kwamba Pesa zinazotolewa kwa walengwa waliopo
kwenye mpango huo zitumike kama ilivyokusudiwa,na hasa kuwekeza kwenye
Elimu,kilimo na mambo mengine ya msingi yatakayosaidia kuwainua kiuchumi.
Mkuu huyo wa mkoa amesema Pamoja na mambo mengine ya msingi
walengwa wa TASAF awamu ya tatu, mpango wa kunusuru kaya masikini,wanapaswa
kuwekeza kwenye Elimu ya watoto wao ili kuwajengea msingi thabiti katika maisha
yao
Kwa upande wao walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini
TASAF awamu ya tatu wilayani kishapu wamesema fedha wanazopatiwa kwenye mpango
huo zimewanufaisha baada ya kuzielekeza katika mambo ya msingi kama vile
ufugaji,kilimo , ujenzi na kusomesha watoto
Post a Comment