Header Ads

MWIZI WA MAJI AKAMATWA TABORA


Image result for PICHA YA Iguwasa


MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa mazingira wilayani Igunga (Iguwasa) mkoani Tabora, imemkamata mkulima akiwa amejiunganishia maji kwa njia ya wizi kwa miaka miwili.

Mkurugenzi wa mamlaka ya majisafi wilaya ya Igunga, Raphael Merumba alikiri kukamatwa kwa mkulima huyo akiwa anatumia maji kwa njia ya wizi pasipo kutumia mita aliyofungiwa na Iguwasa.

Mkulima huyo Mabula Mashenene(50) mkazi wa mtaa wa Stoo wilayani hapa ambaye alikamatwa juzi majira ya saa 2:00 usiku kutokana na msako unaoendeshwa na mamlaka hiyo.

Alibainisha kuwa baada ya kukamatwa mkulima huyo akiwa nyumbani kwake ambapo amelima bustani ya nyanya alikiri kujiunganishia maji mwenyewe kwa njia ya wizi.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo wa Iguwasa aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kukiri mkulima huyo, mamlaka ya maji Igunga imemtoza faini ya Sh milioni 1.7 ikiwa ni pamoja na kumpa onyo la kutorudia tabia hiyo.

Kwa upande wake mkulima huyo Mashenene alipoulizwa na gazeti hili juu ya tuhuma hiyo ya kujiunganishia maji kwa njia ya wizi alikiri kufanya hivyo na kusema kuwa alilazimika kufanya hivyo kwa ajili ya kuokoa mazao yake ya nyanya huku akidai hatarudia tena kosa hilo.



CHANZO HABARI LEO

No comments