kuwauwa watu 27 katika msikiti wa waislam
Mlipuaji mabomu wa kujitolea muhanga amejilipua na kuwauwa watu 27 katika msikiti wa waislam wa madhehebu ya Shia katika mji mkuu wa Afghanstan Kabul, wamesema polisi.
Takriban watu 35 zaidi wamejeruhiwa katika mlipuko huo uliotokeakatika msikiti wa Baqir ul Olum magharibi mwa mji huo.
Shambulio hilo limekuja wakati waumini walipokuwa wamekusanyika kwa sherehe za kidini.
Kundi la Islamic State (IS) limesema kuwa lilihusika na mlipuko huo.
Ni shambulio la hivi karibuni katika ya msururu wa mashambulio kadhaa ya hivi karibuni yanayolenga jamii ya waislam wa madhehebu ya Shia yanayodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kiislam wa madhehebu ya Sunni.
Ulipuaji mabomu huo ulitokea wakati wa ibada ya kumbu kumbu ya kifo cha Imam Hussein, mjukuu wa Mtume Muhammad ambaye pia ni mfiadini wa kishia.
Maafisa wanasema kuwa mshambuliaji alikuwa anatembea kwa miguu na kujilipua miongoni mwa umati wa watu wwaliokuwa nje ya jengo . Walioshuhudia wanasema alijilipua wakati ibada ilipokuwa kalibu kukamilika.
chanzo bbc
Post a Comment