Header Ads

Ukimwi yanachangiwa kwa asilimia 60 na wanaume ambao hawajafanyiwa


Image result for picha ya MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amesema maambukizi ya virusi vya Ukimwi yanachangiwa kwa asilimia 60 na wanaume ambao hawajafanyiwa tohara.

Mtaka aliyasema hayo jana katika kikao cha wadau wa Ukimwi cha kujadili mipango na mikakati mbalimbali ya kudhibiti maambukizi hayo kilichofanyika wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Akifungua mkutano huo, Mtaka alisema maambukizi ya Ukimwi yanachangiwa kwa asilimia 60 kwa wanaume ambao hawajafanyiwa tohara hivyo kusababisha baadhi ya wilaya wenye idadi kubwa ya wanaume wasiofanyiwa tohara kuwa na kasi kubwa ya maambukizi.

Mratibu wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi mkoani hapa, Dk Hamis Kulemba alisema wilaya ya Busega inaongoza kwa asilimia 5.8 ikifuatiwa na Halmashauri ya Bariadi Mjini kwa asilimia 3.8 kwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Alibainisha kuwa mpaka sasa zaidi ya wanaume 138,844 wamefanyiwa tohara kwa kipindi cha miaka miwili ambapo kipindi cha mwaka 2015 wananchi waliopima walikuwa 262,862 na kati ya hao wananchi 8,631 sawa na asilimia 3.3 waligundulika kuwa na maambukizi ya ukimwi.

Mtaka alisema pia wananchi wamekuwa wakiacha kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo, wakijiona wanaendelea vizuri ambapo watu wanaotumia dawa hizo kwa mwaka huu ni watu 40,426 huku wengine wapya 18,246 wamesajiliwa kuanza kumeza dawa hizo.



chanzo habari leo

No comments