Mgomo wa marubani wa Lufthansa umeingia siku yake ya pili hii leo,
copy picha kwenye mtandao
Mgomo wa marubani wa Lufthansa umeingia siku yake ya pili hii leo, huku shirika hilo la ndege la Ujerumani likifuta safari za ndege 912. Hatua hiyo imeiathiri mipango ya usafiri wa karibu abiria 100,000 wa safari za karibu na mbali.
Chama cha Marubani kimetangaza kuwa mgomo huo, wa 14 tangu mzozo huo ulipoanza mwaka wa 2014, utarefushwa hadi siku ya tatu kesho Ijumaa, badala ya siku mbili kama ilivyopangwa awali. Hatua hiyo inayolenga kushinikiza matakwa yao ya nyongeza ya mshahara ya asilimia 22 kwa zaidi ya miaka mitano hadi Aprili 2017, ilisababishwa kufutwa safari za ndege 876 hapo jana.
Kwa jumla, zaidi ya abiria 215,000 wameathirika kwa kipindi cha siku mbili za kwanza.
Post a Comment