Header Ads

SERIKALI imesema itatoa kipaumbele kwa wahitimu kutoka Wakala wa Maendeleo ya Uongozi


Image result for picha ya shule

SERIKALI imesema itatoa kipaumbele kwa wahitimu kutoka Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), katika uteuzi wa viongozi na wadhibiti ubora wa shule ngazi ya Kata na Halmashauri.
Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Raphael Chigunda alisema jana kwenye mahafali ya ADEM, alipokuwa akimwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, MaimunaTarishi yaliyofanyika Bagamoyo, mkoa wa Pwani.

Alisema changamoto kubwa kwa wahitimu hao ni vigezo vya uteuzi ambavyo vinaenda sanjari na viwango vya elimu hivyo aliwataka wasibweteke waendelee kusoma zaidi hadi ngazi ya Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu.
Aliwataka pia wahitimu hao kuwa chachu ya mabadiliko ya uongozi wa elimu pamoja na udhibiti ubora wa shule nchini kwa kutumia ujuzi, maarifa, mwelekeo na mbinu mpya walizozipata katika kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika mitihani.

Kwa upande mwingine alisema, serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imedhamiria kuongeza wigo wa kupata elimu bora nchini, kwani hatua mbalimbali zimeshachukuliwa na utekelezaji wake unaonekana.

Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dk Siston Masanja alisema lengo la wakala ni kuendelea kutoa mafunzo ya cheti cha uongozi na usimamizi wa elimu (CELMA), stashahada ya uongozi na usimamizi wa elimu (DEMA) na stashahada ya ukaguzi wa shule (DSI) kwa viongozi wa idara mbalimbali za elimu nchini.

No comments