SERIKALI imeanzisha utaratibu wa kuharakisha kesi zinazohusu unyanyasaji na ukatili kwa wanawake na wasichama wadogo
SERIKALI imeanzisha utaratibu wa kuharakisha kesi zinazohusu unyanyasaji na ukatili kwa wanawake na wasichama wadogo ili hukumu zitolewe mapema na wahusika watakaokutwa na hatia wafungwe haraka.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati akizungumza baada ya matembezi yaliyoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo (WiLDAF), na mashirika ya kutetea haki za binadamu, ikiwa ni kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza jana hadi Desemba 10.
Waziri Jafo alisema serikali haiwezi kuendelea kuvumilia kuona wanaume wakijihusisha na mapenzi na wasichana wadogo wakati wakiwaacha wanawake wakubwa.
Alisema ingawa sheria imerekebishwa na kuwa kali lakini bado kesi za matukio hayo zimekuwa zikichukua muda mrefu hivyo kuwanyima haki watu waliotendewa matukio ya udhalilishaji wa kingono ama ukatili.
Jafo alisema serikali imeamua kuanzisha utaratibu wa kuharakisha kesi hizo zinapofikishwa kwenye madawati ya jinsia polisi na mahakamani ili hukumu zitoke mapema.
Mratibu wa WiLDAF, Dk Judith Odunga, alisema takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa watoto wa kike wanaacha shule kabla ya kupevuka huku watoto wa kike wakikatisha masomo yao wakiwa shule za sekondari kuliko wa kiume.
Alisema mazingira yasiyo salama kwa shule yana madhara makubwa na kwamba watoto wanapokuwa shule na kufanyiwa ukatili wakingono wako katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya Ukimwi.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Maria Karadenizi alisema matukio ya ukatili dhidi ya wanawake yako kwenye mataifa mbalimbali duniani na jitihada zinahitajika kwa ajili ya kuyamaliza.
Post a Comment