Header Ads

Takribani watu 40 wameuawa baada ya sehemu ya kituo kimoja cha umeme kinachojengwa nchini China kuporomoka.



Image result for picha ya jengo kuwaka moto

Takribani watu 40 wameuawa baada ya sehemu ya kituo kimoja cha umeme kinachojengwa nchini China 
kuporomoka. 

Shirika la habari la Xinhua limesema mnara wa kituo hicho cha eneo la Fengcheng uliporomoka katika saa za alfajiri, na kufunikia chini idadi isiyojulikana ya watu. 

Shughuli ya uokozi inaendelea kwa sasa, ambapo inaripotiwa kuwa karibu watu 68 walikuwa katika eneo hilo la ujenzi wakati ajali hiyo ilitokea. Hii ndio ajali ya karibuni ya viwanda kuikumba nchi hiyo ambayo ina rekodi mbovu ya usalama. Mwezi Agosti, mlipuko wa bomba katika kiwanda cha umeme kinachotumia makaa ya mawe katika mkoa jirani wa Hubei uliwaua watu 21.

No comments