Header Ads

Serikali ya Burundi imekataa kushirikiana na tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa


Image result for picha ya burundi


Serikali ya Burundi imekataa kushirikiana na tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu machafuko ya kisiasa yaliyodumu kwa miezi kadhaa, ikisema tuhuma za ukiukaji zinazotolewa na maafisa wa umoja huo ni sehemu ya njama ya kisiasa.


Umoja wa Mataifa ulitangaza wiki hii kuanzisha uchunguzi wa kuwatambua watuhumiwa katika taifa hilo la Afrika ya Kati, ambalo limekumbwa na machafuko na mauaji tangu maandamano yalipozuka mwaka wa 2015 kupinga uamuzi wa rais kugombea muhula wa tatu. Waziri wa haki za binaadamu wa Burundi Martin Nivyabandi amewaambia waandishi wa habari kuwa sio kwamba wanakataa kushirikiana na tume za haki za binaadamu. 


Wataendelea kushirikiana nao kuhusu masuala mengine lakini hawatakuwa sehemu ya uchunguzi huo. Ripoti iliyotolewa na watalaamu huru iliwataja viongozi wa serikali wanaoshukiwa kuamuru kuteswa au kuuliwa wanasiasa wa upinzani.

Madai hayo yaliikasirisha serikali, ambayo iliwapiga marufuku watalaamu watatu kuingia nchini humo.

No comments