WAHARIFU WA KAMATWA SHINYANGA
Jeshi la
polisi mkoani Shinyanga limewakamata watuhumiwa wapatao 24 ambao wanasadikiwa kujihusisha matukio
mbalimbali ya kihalifu.
Kamanda wa
polisi wa mkoa wa Shinyanga MULIRO JUMANNE MULIRO amesema watuhumiwa hao
wamekamatwa kwa nyakati tofauti kufuatia
misako mbalimbali iliyotokana na taarifa za kiintelejensia ambayo
limeifanya kwa zaidi ya wiki moja.
Amewataja
watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni pamoja na wale wanaohusika katika vitendo vya
uvunjaji,wizi na unyang’anyi,pamoja na kukutwa na pombe haramu ya Ngongo na
dawa za kulevya aina ya bangi.
Kamanda
MULIRO pia ametoa taarifa za kukamatwa kwa watu wawili wanaosadikiwa kuhusika
katika tukio la wizi wa gari lilitokea Septemba nane mwaka huu huko wilayani
MAFINGA mkoani IRINGA, ambapo dereva wa gari hilo aliporwa gari lake baada ya
kuuawa na kisha mwili wake kutupwa kando ya mto RUAHA.
Amesema
watuhumiwa hao wamekamatwa siku ya Novemba 14 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi katika eneo la
BIJAMORA kata ya NYIHONGO wilayani Kahama ,wakiwa na gari hilo aina ya TOYOTA
CARINA lenye namba za usajili T.531 CWA.
Post a Comment