ijiji cha NHELEGANI kata ya KIZUMBI AMANI YA TAWALA
Wakazi wa Kijiji
cha NHELEGANI kata ya KIZUMBI katika manispaa ya Shinyanga wamesema hivi sasa wanaishi
kwa amani baada ya kukoma kwa matukio yaliyokuwa yakihusishwa na imani za
kishirikina ambapo baadhi ya wanawake walilalamikia kuingiliwa kimwili na mtu
asiyejulikana.
Wakizungumza
na KALI ZOTE BLOG baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamebainisha kuwa hivi sasa vitendo hivyo
havitokei kama ilivyokuwa hapo awali na wameiomba serikali kuhakikisha
inachukua hatua za kiusalama zaidi.
Pamoja na
madai hayo ya wananchi Mwenyekiti wa kijiji hicho cha NHELEGANI Bw.SENI SHIJA
amendelea kukanusha kuwepo kwa matukio hayo na baada ya kuhojiwa zaidi na
waandishi wa habari alikataa kuzungumza.
Siku chache
zilizopita wananchi wa vijiji vya NHELEGANI na BUGAYAMBELELE kata ya kizumbi
katika manispaa ya Shinyanga walilalamikia kuibuka kwa mtu ambaye alikuwa
akiingia kimazingara katika nyumba zao nyakati za usiku na kisha kuchukua vitu
mbalimbali ikiwemo fedha na simu za mkonani na baadaye kuwaingilia kimwili
baadhi ya wanawake.
Post a Comment