zaidi ya watu themanini wameuawa kwa shambulizi la bomu
Vyombo vya usalama vya Iraq vimesema kwamba zaidi ya watu themanini wameuawa kwa shambulizi la bomu lililowalenga madhehebu ya kiislamu ya kishia kusini mwa mji wa Baghdad.
Gari lililokuwa limebeba vilipuzi hivyo lililipuka karibu na kituo cha mafuta ambapo watu wengi wa dhehebu hilo walikuwa wameegesha magari yao.
Wengi wa watu waliofariki ni wananchi wa Iran na Afghanistan.
Walikuwa wakitoka kwenye moja ya tukio muhimu la kidini kwenye mji mtakatifu wa Karbala.
Askari wa kundi la kiislam wamekiri kuhusika na shambulizi hilo.
kundi hilo la wapiganaji la kiislam mara kwa mara hulenga madhehebu ya kishia na kuwatuhumu kwamba ni waongo.
Post a Comment