LIBERATUS SANGU amewataka wanafunzi waliomaliza masomo katika Seminari ya awali ya Sayusayu kuwa mfano mzuri kwa wengine
Askofu wa Jimbo katoliki la Shinyanga mhashamu LIBERATUS SANGU amewataka wanafunzi
waliomaliza masomo katika Seminari ya awali ya Sayusayu kuwa mfano mzuri kwa
wengine, kutenda mema na kuonyesha upendo kwa wengine
Akizungumza katika Misa maalumu ya mahafali ya 13,ya Seminari
hiyo askofu SANGU amewataka wanafunzi waliohitimu masomo ya mwaka mmoja katika
Seminari hiyo kuendelea kuishi maisha ya kumfuata kristu kwa kuonesha
upendo,usiokuwa na Mipaka,hata kwa wale wasiokuwa wakristu,na kuwa chimbuko la
kupunguza mateso kwa wengine.
Aidha amewaomba waamini kuendelea kuwaombea waseminari hao
ili wale wanaotamani wito wa upadri waweze kufikia,na kwamba anaamini miongoni
mwao wapo watakaofikia daraja takatifu
la uaskofu,na wengine kuwa na nyadhifa mbalimbali katika kanisa
Jumla ya wahitimu 284 wamemaliza masomo yao ya mwaka mmoja
katika Seminari ya awali ya mtakatifu
Gregory mkuu iliyopo Sayusayu
wilayani Maswa mkoani Simiyu,ambao wanatoka katika majimbo matano yaliyopo
kanda ya ziwa,ikiwemo Jimbo la Shinyanga,Mwanza,Geita,Bunda,na Musoma.
Baada ya masomo hayo waseminari hao wataanza masomo ya kidato
cha kwanza mnamo Januari mwaka kesho,katika Seminari ndogo za
Shanwa,Makoko,Nyegezi,na Sengerema
Post a Comment