gari laponda nyumba old shinyanga
Mtu mmoja
aitwaye JULIUS MWANDU mkazi wa OLD
SHINYANGA katika manispaa ya Shinyanga imenusurika kifo baada ya Lori la
kusomba mchanga kuparamia nyumba yake wakati akiwa amelala.
Tukio hilo
limetokea leo majira ya saa mbili asubuhi baada ya tela la gari hilo lililokuwa
likimwaga mchanga jiarani na nyumba yake kufyatuka na kuaparamia sehemu ya
nyumba hiyo.
Kwa mujibu
wa watu walioshuhudia tukio hilo wamesema tela la gari hilo lilifyatuka na
kuingia katika chumba alichikuwa amelala Bw.JULIUS lakini alifanikiwa kutoka
kabla ya ukuta wa nyumba kuanguka.
Hakuna mtu
aliyejeruhiwa katika tukio hilo ingawa baadhi ya vitu ikiwemo baiskeli na kitanda vimeharika vibaya baada
ya kupondwa na na ukuta wa nyumba.
Dereva wa
gari hilo lenye namba za usajili T.821 AYM alifanikiwa kukimbia mara baada ya tukio
hilo kutokea.
Mwenyekiti
wa kijiji cha OLD SHINYANGA DOTTO BWIRE amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
nyumba ya juliasi mwandu
gari lilolo anguka
Post a Comment